We use cookies to enhance your user experience. By continuing to visit this site you agree to our use of cookies.
0
Posts
0
Followers
0
Following
Kuhusu Moshibiz Blog Karibu Moshibiz Blog — kituo chako namba moja cha habari za biashara, ujasiriamali, fursa za kiuchumi, na maendeleo ya jamii. Lengo letu kuu ni kuwainua wajasiriamali, vijana, na jamii kwa ujumla kwa kuwapatia taarifa sahihi, elimu ya biashara, na fursa mpya zinazoweza kubadilisha maisha yao. Tunaamini kuwa kwa kupata taarifa sahihi kwa wakati, kila mtu ana uwezo wa kuanzisha na kukuza wazo lake la biashara. Dira Yetu (Vision) Kuwepo kama chanzo kikuu na cha kuaminika cha taarifa za kibiashara na fursa za kiuchumi Mkoani Kilimanjaro na Tanzania nzima. Dhamira Yetu (Mission) Kuelimisha, kuhamasisha, na kuunganisha jamii na fursa za kibiashara, ajira, masoko, na mbinu za kisasa za ujasiriamali kupitia maudhui ya kidijitali yanayoeleweka kwa urahisi. Tunachokufanyia: Elimu ya Biashara na Ujasiriamali: Mbinu za kuanzisha, kuendesha, na kukuza biashara ndogo na za kati. Fursa za Masoko na Uwekezaji: Taarifa kuhusu fursa mpya za kibiashara zilizopo Moshi na maeneo jirani. Tangazo la Biashara Yako: Kuunganisha wafanyabiashara na wateja kupitia matangazo na makala za kukuza bidhaa au huduma. Habari na Matukio ya Kibiashara: Updates za matukio yote muhimu ya kiuchumi na maonyesho ya biashara. Mawasiliano jukwaa la kidijitali linaloangazia fursa za kibiashara, ujasiriamali, ajira, elimu, na habari mbalimbali za maendeleo, hasa zikijikita katika Mkoa wa Kilimanjaro (Moshi) na Tanzania kwa ujumla.